*Kwa wanaotaka kujiunga elimu ya juu* , wengi huwa hawajui kozi wanazotaka kusoma zina mwelekeo upi. Wengi pia hata vyuo wanavyotaka kwenda kuvisoma hawavijui vizuri. Wale wanaopata bahati ya kuelezwa vizuri, huenda vyuo bora na kozi bora zenye matokeo chanya wamalizapo chuo. Ndio maana walio wengi siku hizi huaplai Chuo Kikuu Ardhi (Ardhi University). Unaweza kuaplai moja kwa moja mtandaoni
(http://aru.admission.ac.tz).
Chuo Kikuu Ardhi ni moja ya vyuo vikuu vikongwe zaidi Tanzania. Kwa hatua mbalimbali kilichopitia, kina zaidi ya miaka sitini. Idadi ya waombaji inaendelea kuongezeka mwaka hata mwaka, kwa vile siku hizi vijana wengi hawaendi kusoma digirii kwa sifa tu kwamba na mimi niko chuo, bali huangalia mbali zaidi ya hapo.
Hapa chini, ni maelezo kwa ufupi kuhusu kozi za digirii zilizoko Ardhi University, muda wa kozi, na nafasi za kujiunga zilizoko. Maelezo zaidi utayaona http://www.aru.ac.tz . Kuaplai moja kwa moja ni kupitia http://aru.admission.ac.tz
1. Kozi za Usanifu majengo - majengo yenyewe, ndani ya majengo au nje ya majengo. Tanzania bado ina uhaba mkubwa wa wasanifu majengo. Kozi hizi ni nzuri sana kwa kujiajiri na kuajiriwa.
AR001 *Bachelor of Architecture* Five years. 45 students.
AR002 *Bachelor of Science in Interior Design* Four years. 30 students.
AR003 *Bachelor of Science in Landscape Architecture* Four years. 25 students.
*ENTRY REQUIREMENTS*
Two principal passes in any of the following: Mathematics, Physics, Chemistry, Biology, Geography or Fine Art. If one of the principal passes is not Mathematics, a subsidiary pass in Advanced Mathematics/Basic Applied Mathematics or credit pass in O-level Mathematics is required.
2. Kozi upimaji ardhi (Masorovea au Wapima, a.k.a wasaka nyoka). Asilimia kubwa ya nchi hii haijapimwa... Wanafanya kazi kwenye ujenzi, migodini, kuchora ramani... Kwenye halmashauri utawakuta kwenye idara ya upimaji ardhi na ramani.
AR004 *Bachelor of Science in Geoinformatics* Four years. 35 students.
AR005 *Bachelor of Science in Geomatics* Four years. 55 students.
*ENTRY REQUIREMENTS*
A principal pass in Mathematics and either Physics or Chemistry or Geography or Computer Science. If one of the principal passes is not Physics, at least a subsidiary pass in Physics at A’ level is required.
3. Kozi ya ukadiriaji thamani gharama za ujenzi ( _Quantity Surveying_ , QS). Wahitimu wa kozi hii ni muhimu sana. Hawavumi lakini wamo. Hawa huwa ni wanaoandaa makadirio ya majenzi ya majengo, barabara na mengineyo. Hufuatilia masuala ya mikataba katika ujenzi. Usibabaishwe na "Economics" kwenye jina la kozi... kozi hii ni ya kisayansi zaidi. Angalia entry requirements zake:
AR006 *Bachelor of Science in Building Economics* Four years. 65 students.
*ENTRY REQUIREMENTS*
Two principal passes in any of the following: Mathematics, Physics, Chemistry, Geography, Economics or Accounts. In addition, a candidate must have at least a subsidiary pass in Advanced Mathematics/ Basic Applied Mathematics and at least a pass in Physics at O-level.
4. Kozi za utaalamu wa Mazingira. Hizi ndio usiseme! Yaani wahitimu wa hizi kozi ni 'viraka' -- wanafiti nafasi mbalimbali za utaalamu kwa vile mazingira ni kila kitu kinamchomhusu binadamu, akiwemo binadamu mwenyewe. Huhusika kufanya tathmini za mazingira (EIA), mazingira bora maeneo ya kazi (Occupational Health), uhandisi mazingira, maji safi na maji taka, nasuala ya taka ngumu, uchafuzi wa hali ya hewa, climate change, mambo ya disaster risk management, nini tena hawamo wataalamu wetu hawa?
AR009 *Bachelor of Science in Environmental Engineering* Four years. 75 students.
AR014 *Bachelor of Science in Municipal and Industrial Services* Four years. 25 students.
*ENTRY REQUIREMENTS*
Two principal passes in any of the following; Mathematics, Physics, Biology or Chemistry. If the two principal passes are not Mathematics and Physics, an applicant must have at least a ubsidiary pass in Physics and Advanced Mathematics/Basic Applied Mathematics.
AR011 *Bachelor of Science in Environmental Science andManagement* Four years. 85 students.
*ENTRY REQUIREMENTS*
Two principal passes in any of the following; Mathematics, Physics, Geography, Biology or Chemistry. One of the two principal passes must be either Physics, Chemistry or Biology. If one of the principal passes is not Mathematics, a subsidiary pass in Advanced Mathematics/Basic Applied Mathematics is required.
4. Masuala ya Makaazi. Mahitaji ya nyumba na makazi yanazidi kuongezeka kila uchwao. Kila siku wanazaliwa maelfu ya watu. Kila mwaka ni vijana wangapi wanaoamua "kuanza maisha"? Wote hawa huingia kwenye soko la makaazi. Hawa wataalamu wa masuala haya wataendelea kuhitajika zaidi. Humo wamo wenye kupanga mipango ya aina mbalimbali, ikiwemo mipango miji na vijiji, uandaaji matumizi bora ya ardhi, nk. Kwenye halmashauri hawa ndio utawakuta ni maafisa mipango miji.
AR012 *Bachelor of Science in Housing and Infrastructure Planning* Four years. 25 students.
AR016 *Bachelor of Science in Regional Development Planning* Four years. 25 students.
AR018 *Bachelor of Science in Urban and Regional Planning* Four years. 55 students.
*ENTRY REQUIREMENTS*
Two principal passes in any of the following: Physics, Chemistry, Biology, Geography, Economics, History, Mathematics, Commerce or Accountancy. If one of the principal passes is not Mathematics, a subsidiary pass in Advanced Mathematics/Basic Applied Mathematics or at least a pass in mathematics at O’ level is required.
5. Kozi za masuala ya miliki. Hawa ni wale mavalua, wanaokadiria thamani za majengo yaliyokamilika. Ni wataalamu wa ardhi, valuation of company assets, viwanja, estate management, na kadhalika. Kwenye halmashauri utawakuta ndio Maafisa Ardhi, mavalua, na vyeo vinginevyo.
AR013 *Bachelor of Science in Land Management and Valuation* Four years. 125 students.
AR015 *Bachelor of Science in Property and Facilities Management* Four years. 35 students.
AR017 *Bachelor of Science in Real Estate* Four years. 35 students.
*ENTRY REQUIREMENTS*
Two principal passes in any of the following; Geography, Economics, Mathematics, History, Commerce, Accountancy, English Literature, Physics, Biology or Chemistry. If one of the principal passes is not Mathematics, a subsidiary pass in Advanced Mathematics /Basic Applied Mathematics or at least a pass in O’ level Mathematics is required.
6. Kozi mahususi. Hizi kozi mbalimbali zinawawezesha wahitimu kuwa magwiji kwenye taaluma zao. Hapo tunapata
A. Wachumi (Economists). Hawa ni watu wa mipango na mipangilio ya maendeleo ya taasisi anuai.
B. Wataalamu wa Menejimenti ya Mifumo ( _Information Systems Management_ ). Hii ni kozi safi sana kwa wale wenye kupenda kutumia kompyuta kutatua matatizo ya taarifa. Wapi wasipotumia kompyuta? Hawa wanafiti kila mahali. Na ni wachache sana, hasa ukitilia maanani nchi yetu bado inahamia kwenye mifumo ya kidijitali toka ile ya analogia. Ni kama sehemu mahususi ya Computer Science ambayo nadharia ni kiasi, lakini utendaji ndio mwingi (application) wenye kutatua shida halisi, siyo za kinadharia.
C. Wahandisi ujenzi (Civil Engineers). Hawa ndio wanaofanya uhandisi wa masuala kedekede ya ujenzi wa uimara wa majengo, kusimamia na kutekeleza kandarasi za ujenzi wa majengo, barabara na vyote vingine vinavyohitaji utaalam wa kujenga.
D. Wahasibu na Wataalam wa Fedha. Hii kozi ni ya kipekee miongoni mwa zile za uhasibu Tanzania kwani Wahitimu wa kozi hii wamekuwa wakitafutwa sana na waajiri kutokana na weledi wao.
E. Wataalamu wa maendeleo ya jamii ( _community and development_ ). Hawa wanaenda kutekeleza miradi iliyoko kwenye jamii. Miradi siku hizi huhusisha ushirikishwaji umma. Hushiriki pia kwenye tathmini za mazingira (EIA) pamoja tathmini na tafiti zingine. Kwenye halmashauri ndio maafisa maendeleo.
AR019 *Bachelor of Arts in Economics* Three years. 95 students.
AR020 *Bachelor of Science in Information Systems Management* Three years. 55 students.
AR021 *Bachelor of Science in Civil Engineering* Four years. 60 students.
AR022 *Bachelor of Science in Accounting and Finance* Three years. 110 students.
AR023 *Bachelor of Arts in Community and Development Studies (CDS)* Three years. 95 students.
*ENTRY REQUIREMENTS*
AR019 *Bachelor of Arts in Economics*
Two principal passes in any of the following: Physics, Chemistry, Mathematics, Geography, Economics, History, Commerce or Accountancy. If one of the principal
passes is not Mathematics, a subsidiary pass in Advanced Mathematics /Basic Applied Mathematics or at least a credit pass in Mathematics at O’ level is required.
AR020 *Bachelor of Science in Information Systems Management*
Two principal passes in any of the following: Mathematics, Physics, Geography, Chemistry, Economics or Computer Science. If one of the principal passes is not
Mathematics, an applicant must have at least a subsidiary pass in Advanced Mathematics /Basic Applied Mathematics.
AR021 *Bachelor of Science in Civil Engineering*
Principal passes in Mathematics and Physics. Those without a subsidiary pass in Chemistry at A’ level must have a credit pass in Chemistry at O’ level
AR022 *Bachelor of Science in Accounting and Finance*
Two principal passes in any of the following: Commerce, Accountancy, Economics,
History, Geography, Mathematics, Physics, Biology or Chemistry. In addition, at least a subsidiary pass in English Literature and Mathematics/Basic Applied Mathematics at Alevel or a pass in English and Mathematics at O-level is required.
AR023 *Bachelor of Arts in Community and Development Studies (CDS)*
Two principal passes in any of the following: Physics, Biology, Chemistry, Mathematics, Geography, Economics, History, Commerce, Accountancy, Agricultural Science or
Nutrition.
Kozi zote hizo ziko http://aru.admission.ac.tz
*SHARING IS CARING*