-->

HESLB IN FINAL PREPARATION TO OFFER LOAN 2017 /2018

- July 25, 2017
Wakuu na maafisa wa Idara na Vitengo mbalimbali vya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu wapo katika maandalizi ya mwisho ya kufanyia majaribio mfumo wake ulioboreshwa wa uombaji mikopo kupitia olas.heslb.go.tz kabla ya kukaribisha maombi ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/2018.


OLAMS

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa TEHAMA Bw. Muze Ninkhambazi ambaye ameongoza mafunzo ya kuwapitisha idara na vitengo hivyo ili kuufahamu na kupata mapendekezo kutoka kwao kwa ajili ya kuboresha mambo muhimu yanayoingia katika mfumo huo kabla ya kukaribisha maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
Bw. Ninkhambazi amesema mabadiliko ya mfumo yanalenga kuufanya uwe wa kisasa zaidi na kuwarahisishia waombaji mikopo jinsi ya kuwasilisha taarifa zao Bodi. Aidha ameongeza kuwa maandalizi hayo yamewezesha kupata mchango mkubwa kutoka wa washiriki.


Miongoni mwa mabadiliko katika OLAMS ni pamoja na jinsi ya kufanya malipo, kuwasilisha viambatanisho muhimu kama cheti cha kuzaliwa, cheti cha kidato cha nne na saini za mwombaji na mdhamini wake.
Bodi ya Mikopo iliingia katika mfumo wa uombaji mikopo kwa njia ya mtandao mwaka wa masomo 2010/2011 na tangu wakati huo mfumo huo umekuwa ukiboreshwa ili kuendana na teknolojia mpya.

Source click here